Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kuhusu mkutano wa baadhi ya wasanii na waigizaji maarufu wa Nigeria – ambao miongoni mwa kazi zao ni kuigiza katika filamu ya "Hausa" – na kiongozi wa Harakati ya Kiislamu Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky, katika makazi yake yaliyopo Abuja.
Wageni hawa wametaja lengo lao la ziara hii kuwa ni kupata mwongozo na ushauri kutoka kwake juu ya namna ya kuendeleza shughuli zao ili ziweze kuchangia katika kukuza zaidi maadili na thamani ya Kiislamu.
Miongoni mwa wosia wa Sheikh Zakzaky kwao ilikuwa kwamba: “Kila mmoja wenu anatakiwa kuwa balozi wa Uislamu wa kweli; katika uzalishaji wa maudhui ya burudani, elezeni thamani ya uislamu. Kuzalisha maudhui ya burudani yenye thamani ndilo jambo muhimu zaidi katika sekta ya burudani ya leo.”
Maoni yako